Steven Mgeni
Sunday, November 4, 2012
Thursday, May 26, 2011
WATANO WATIWA MBARONI TUNDURU
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia wawindaji haramu watano Wakazi wa Kijiji cha Mwambesi kilichopo Wilayani Tunduru kwa tuhuma za kukutwa na vipande ishirini vya nyama ya kiboko yenye thamani ya shilingi milioni 4.331800 , mitego 11 ya kutegea wanyama na wengine wanasakwa kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo 36 yenye uzito wa kilo 75.75 pamoja na nyama ya vipande 7 vya nyama ya nyati vyenye uzito wa kilo 4 na singa 3 za tembo.
Akizungumza jana ofisini kwake kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amelitaja tukio la kwanza kuwa lilitokea mei 23 mwaka huu majira ya saa za asubuhi katika mbuga ya hifadhi ya Taifa ya wanyama iliyopo eneo la Mwambesi ambako askari wakiwa doria waliwakamata wawindaji haramu wakiwa na vipande 20 vya nyama ya kiboko pamoja na mitego 11 ya kutegea wanyama.
Waliokamatwa wametajwa kuwa ni Makosa Masanyata (45),Salumu Saidi (30),Salumu Yakubu (25),Galaus Halifa na Alphonce Najidi (45) wote wakazi wa Kijiji hicho ambao kwasasa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Kamuhanda alilitaja tukio jingine kuwa lilitokea mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku huko kwenye eneo ya njia panda yakwend kijiji cha masonya lililopo katika kijiji cha Nakayaya wilayani Tunduru akari wa Idara ya wanyama pori toka kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya kusini wakiwa na pikipiki walikutana na gari aina ya saloon amabyo waliitilia mashaka.
Alisema kuwa askari hao baada ya kuitilia mashaka gari hiyo walianza kuikimbiza lakini kwa vile kulikuwa na vumbi jingi walishindwa kuipata baada ya gari hiyo kukatisha njia na wao kupitiliza hadi Tunduru mjini ambako walijaribu kuitafuta hawakuipata.
Alifafanua zaidi kuwa askari hao baadaye walilazimika kurudi tena kwenye eneo la njia panda lililopo kwenye njia panda ya kwenda masonya kijiji cha Nakayaya na kuanza kuifuatilia gari hiyo kwa kuangalia taili za gari na baadae walifanikiwa kufika mwisho ambako taili zinaonyesha zimeishia kwenye kichaka ambako walikuta meno ya tembo 36 yenye uzito wa kilo 75.75, vipande saba vya nyama ya nyati vilivyokaushwa vyenye uzito wa kilo nne na singa 3 za temb.
Alibainisha kuwa thamani ya nyara zote za Serikali zilizokamatwa ni US $ 274000 sawa na fedha za kitanzania sh.402784000 na kwamba polisi bado inaendelea kuwasaka wawindaji haramu ambao walizificha nyara hizo kwenye kichaka na kutokomea kusiko julikana
MWISHO.
Friday, May 20, 2011
Saturday, February 5, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)